Watu 100 Ndio Watakaoruhusiwa Kuhudhuria Ibada

  • 4 years ago
Baraza la kidini linaloongozwa na kasisi Anthony Muheria limependekeza kufunguliwa kwa maeneo ya ibada jumanne wiki ijayo. Katika hotuba yake muheria amesema maeneo hayo yatafunguliwa kwa awamu na idadi ya watakaoruhusiwa kwa wakati mmoja kuhudhuria ibada hawatazidi 100 kama ilivyoelekezwa na rais Uhuru Kenyatta. Tayari viongozi mbali mbali wameibua hisia zao kuhusiana na mikakati iliyowekwa kufunguliwa kwa maeneo ya ibada