PIGO BAYA Kwa Mbowe na CHADEMA Siku ya leo limewakuta

  • 6 years ago
Wakili Jeremiah Mtobesya anayewatetea viongozi tisa wa Chadema akiwamo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amejitoa kwenye kesi hiyo.

Mtobesya amechukua uamuzi huo leo Agosti 23 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili huyo alijitoa kuwatetea washtakiwa hao mara baada ya Mahakama ya Hakimu Kisutu kuyatupilia mbali maombi yao ya kutaka kesi hiyo ya jinai namba 112 ya mwaka huu iahirishwe katika Mahakama ya Kisutu ili kusubiri maombi yao na rufaa yaliyopo Mahakama ya Rufani yasikilizwe na kutolewa maamuzi.

Hata hivyo Hakimu Mashauri aliyatupilia mbali maombi hayo kwa sababu kifungu cha sheria walichotumia cha 225 (1) (2) cha Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho2002 hakiipi mamlaka hayo.

Viongozi hao tisa wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwamo kuhamasisha maandamano Februari 16 mwaka huu siku moja ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni.

Usipitwe na Matukio Muhimu kutoka Kenya, Tanzania na Uganda kwa Lugha ya Kiswahili katika channel hii. Subscribe sasa na bofya alama ya kengere inayotokea baada ya Subscribe. Fungua Link hii .

Recommended