Maisha Peupe: Looking after the Old

  • 12 years ago
Ni mara ngapi tunajihusisha na shughuli zetu za kawaida na kusahau kuwatunza wazazi wetu au nyanya na babu zetu ambao wametimiza miaka ya uzeeni na wanatuhitaji zaidi kuwatunza na kuwashughulikia?
Ndio hali aliyojipata kwayo Joyce Wanjiku aliyeeleza KTN kuwa alijitosa mno ndani ya kazi yake nje ya nchi kiasi cha kukosa kumhudumia mamake namna alivyostahili kuhudumiwa hadi pale mamake alipoaga dunia na kumuacha bi Joyce na majonzi tele.
Ni tukio lililomfanya joyce wanjiku kuanzisha shirika la kuwahudumia wakongwe katika eneo la mweiga nyeri na viunga vyake kwa heshima ya mamake marehemu purity Wanjiru. Ijumaa iliyopita ulimwengu uliadhimisha siku ya uhamasishaji dhidi ya dhuluma kwa wakongwe ambapo tunahimizwa kuwakumbuka wakongwe wanaotuhitaji. Huyu hapa carol nderi na makala ya wiki hii ya maisha peupe.

Recommended