Timu Ya Taifa Ya Kinadada Ya Voliboli Ya Ufuoni Yazabwa Na Marekani

  • 3 years ago
Vipusa Wa Kenya Katika Voliboli Ya Ufukweni Wameshindwa Mechi Ya Pili Ya Kundi D Katika Michezo Ya Olimpiki Baada Ya Kunyukwa Seti 2-0 Na Usa Mapema Alhamisi. Timu Ya Kenya Inayowajumuisha Gaudencia Makokha Na Brackside Khadambi Ilishindwa Seti Ya Kwanza Alama 21-8 Na Kulemewa Zaidi Katika Seti Ya Pili Wakishindwa 21-6, Ikiwa Mechi Ya Pili Mtawalia Kushindwa Baada Ya Kuzidiwa Maarifa Na Brazil Katika Pambano La Ufunguzi.Kenya Watarejea Uwanjani Tarehe 31 Mwezi Huu Dhidi Ya Latvia Katika Mechi Ya Kukamilisha Ratiba.Kenya Inashiriki Olimpiki Katika Mchezo Huo Kwa Mara Ya Kwanza.

Recommended