Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”

  • 5 years ago
Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”
Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.”

Tazama Zaidi:
Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu" https://sw.kingdomsalvation.org/videos/understand-God-s-disposition-word.html

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Baadhi ya vifaa ni kutoka:
http://www.greenmountaindrone.com

Recommended